Tuesday, March 31, 2015

Msanii KEISHA apata ajali akitokea chuoni CBE




Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba, Posta jijini Dar.
Akizungumza na Clouds Fm alisema kuwa alikuwa akitoka chuoni CBE na kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo ndipo lilipotokea gari na kumuovateki na kuligonga gari lake. Aidha alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani.
“Nashukuru Mungu nilipimwa hospitali vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote kwa ndani kwani nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa ndani
dani,” alisema Keisha

Thursday, March 5, 2015

Nuh Mziwanda Anusurika Kupigwa Chupa na Shilole ambaye ni Mpenzi Wake





Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.

Katika tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda,ghafla sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa chupa ambayo ilikuwa ikimlenga msanii huyo bahati nzuri aliikwepa ikampiga jamaa mmoja lakini haikumjeruhi.

Baada ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie juu Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua kukaa pembeni peke yake na kuanza kulia.

 ‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli alileta fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu walikuwa kwenye sherehe hiyo.



Baada ya hapo msanii Quick Racka alimfuata Shilole na kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia chupa ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye aliikwepa ikapasuka chini.

Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu Shilole kumsomea mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo alikuwa amelala.

Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh Mziwanda kwa kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi karibuni alimpiga vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za viwanja vya Leaders na baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia vyombo vya habari na kuahidi kutompiga tena.

Nguo Fupi Yamdhalilisha......Wanaume Wakware Wamshambulia, Aokolewa na Boda boda






Hiyo ni Picha ya Msichana ambayo siku ya jana imesambaa sana mitandaoni...

Inasemekana alipita maeneo ya Sinza akiwa amevaa kinguo kifupi ambacho kilivuta hisia za wanaume  wakware na kuanza kumzonga zonga wakitaka kumvua kabisa kimini hicho huku wengine wakimchoma vidole sehemu zake za siri.

Kwa bahati nzuri alitokea  boda boda na kuamua kumsaidia kwa kumpakia na kutimua mbio.






Tuesday, March 3, 2015

Kodi Yamkimbiza Mama Kanumba Sinza



  
MAMA mzazi wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amefunguaka baada kuongea na FC kuwa moja ya sababu iliyofanya ofisi yake kuhama kutoka maeneo ya Sinza Meeda ilipokuwa wakati wa uhai wa mwanaye ni gharama za pango hilo kupanda kila mwaka.

“Kuna watu ambao wanadai na kuandika hata katika mitandao ya kijamii kuwa eti ofisi za Kanumba The Great Films zimefungwa na hazipo tena, si kweli kodi ni kubwa sana hivyo tumehamishia Kimara Temboni,”anasema Mama Kanumba.

Mama Kanumba amesema kuwa ofisi hiyo inafanya kazi wala haijafungwa na kwa uhakika ni kwamba kuna filamu ambayo imekamilika na itatoka hivi karibuni chini ya kampuni, filamu hiyo imewashirikisha wasanii Flora Mtegoa, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Rose Ndauka na wasanii wengine