Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles
Tizeba akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Chuo cha
Bahari Dar es Salaam (DMI), mara baaada ya kuwasili chuoni hapo
kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho na kuongea na
wafanyakazi wa Chuo hicho, mwanzoni mwa wiki. Kulia kwake anaemtazama ni
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Kapteni Yasin Songoro.
Mkufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam
(DMI), akimpa maelezo ya namna ambavyo wahandisi wanaofanya kazi ndani
ya chumba cha injini ndani ya Meli wanavyoendesha mitambo hiyo kwa Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, wakati alipotembea
chuoni hapo mwanzoni mwa wiki kuongea na wafanyakazi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Charles Tizeba, akimsikilza Kapteni Jumanne Karume, alipokuwa akimpa
maelezo ya namna nahodha anavyoendesha Meli, wakati alipotembelea Chuo
Cha Bahari Dar es Salaam(DMI), mwanzoni mwa wiki. Kushoto kwa Dk Tizeba
ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Kapteni Yasin Songoro.
Naibu Waziri wa Wizara ya
Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (aliyeweka mikono mfukoni), akimsikiliza
Kapteni Peter Mkunja wakati akimpa maelezo ya namna vyombo vya kujiokoa
vinavyotumika endapo meli itazama ama kupata hitilafu yoyote, wakati
Naibu Waziri huyo alipotembelea Chuo hicho Mwanzoni mwa wiki.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar
es Salaam (DMI), Kapteni Yasin Songoro, akitoa maelezo ya namna ambavyo
mashine inayotengeneza vipuri vinayoharibika ndani ya meli inavyofanya
kazi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba,
alipotembelea Chuoni hapo Mwanzoni mwa wiki hii.
Sehemu ya Menejimenti na
wafanyakazi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (Hayupo Pichani),
wakati alipoongea nao mwanzoni mwa wiki.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
No comments :
Post a Comment