Saturday, February 7, 2015

UZINDUZI WA CD YA KWAYA YA UKWATA KUTOKA CHUA CHA UALIMU BUSTANI KILICHOPO MKOANI DODOMA

UKWATA kama chama cha dini cha vijana katika chuo cha ualimu BUSTANI kilichopo wilayani kondoa mkoani DODOMA watazindua CD yao ya nyimbo za dini iitwayo FURAHINI KATIKA BWANA AMBAYO ITAZINDULIWA TAREHE 8/2/2015 katika kanisa la K.K.K.T lililopo kondoa mjini kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni. WOTE MNAKARIBISHWA KATIKA UTUMISHI WA MUNGU.






Wednesday, February 4, 2015

Kitendo ya Dada yake Diamond Kudendeka na Wema Chawa Gumzo Mtandaoni



Siku za hivi karibuni kumeibuka na mtindo mpya wa watu kulishana keki wa kutumia mdomo yaani “Kudendeka”.

Picha ya mrembo na mwigizaji wa filamu  Wema Sepetu akilishwa keki kwa mdomo na dada yake Diamond, Esma imeibua mjadala mtandaoni baada ya baadhi ya watu kudai kuwa Wema anataka kumrusha roho Zari ambae awari aliandika ujumbe mtandaoni na kumuita Esma WIFI. Huku wengine wakiona kama ni kawaida kwani kwa kiasi kikubwa Wema ndio aliewawezesha Esma na Petti Man wakafunga ndoa.

Tukio hilo lilifanyika hivi majuzi, kwenye Birthday Party ya Esma iliyofanyika Samaki Samaki, Masaki.

Mastaa kadhaa wa hapa Bongo walitokea kwenye pati hiyo wakiwemo, Aunty Ezekiel, Queen Dorleen,Mirror na wengine wengi.

Jionee Badhi ya picha za kwenye pati hiyo hapo juu.