Friday, April 3, 2015

Al-Shabaab washambulia chuo kikuu Kenya. Watu 15 wauawa. Washikilia mateka ndani. Warushiana risasi na Polisi, jeshi


Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wavamia na kushambulia Garissa University iliyopo katika mji wa Garissa. Mpaka sasa, watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 60 wamejeruhiwa.


Mmoja wa majeruhi akikimbizwa hospitali
Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi. Polisi waliokuwepo chuoni hapo wakilimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.


Wanafunzi walionusurika wakikimbia kutoka katika eneo la tukio
Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia, na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, na polisi na wanajeshi. Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana. Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano, na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.


Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani

Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao

Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho

Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa













No comments :

Post a Comment