Wednesday, December 17, 2014

HUU NDIO UKWELI WA ASILIMIA 90 KUHUSU KIFO CHA AISHA MADINDA

…aliondoka nyumbani jana na hakurudi tena, madawa ya kulevya yahusishwa

Kifo cha mnenguaji Mwainaisha Mohamed Mbegu “Aisha Madinda” aliyefariki leo, kimeleta utata kwa namna kilivyotokea.
Saluti5 inakuletea kwa muhtasari wa namna kifo cha Aisha Madinda kilivyotokea, hii ikiwa ni kwa mujibu wa ndugu na marafiki wa marehemu waliokusanyika hospitali ya Mwananyamala hadi muda huu.
Mtoto wa kwanza wa marehemu, Feisal ameiambia Saluti5 mama yake ambaye alikuwa haumwi chochote, aliondoka nyumbani juzi na hakurejea tena.
Feisal anasema jana aliongea na mama yake kwa njia ya simu kwa zaidi ya mara tatu na akamwambia yuko Mabibo kwa rafiki yake aitwaye Samira.
Lakini Samira anasema Aisha Madinda hakuwa kwake hiyo jana lakini alimkuta barazani kwake (Mabibo) asubuhi ya leo akiwa hajitambui.
Samira anasema alijitahidi kumtingisha lakini Aisha Madinda alikuwa kimya na hivyo akaamua kuchukua bajaji na kumkimbiza hospitali ya Mwananyala.
Rafiki huyo wa Aisha Madinda anasema alifika Mwananyamala Hospitali majira ya saa 2 asubuhi na daktari aliyempokea akamwambia tayari mgonjwa wake alishafariki dunia.
Samira anasema, yeye kama alivyo Aisha Madinda, ni muathirika wa madawa ya kulevya ambapo anaitaja hospital ya Mwananyamala ndio kliniki yao ya kupata tiba saidizi (MAT) ya madawa ya kulevya na ndio sababu hakumpelekea hospitali nyingine yoyote zaidi ya Mwananyamala.
Kinachoshukiwa:
Marafiki wa Aisha Madinda ambao nao ni waathirika wa madawa ya kulevya, wanadai Aisha Madinda alirudia utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo wana mashaka kuwa alitumia kiasi kikubwa kuliko inavyohitajika na pengine ndio sababu ya kifo chake.
Ndugu wanasemaje?
Ndugu wa marehemu akiwepo dada yake ambaye ndio wa kwanza kuzaliwa, Amida Mohamed Mbegu, ameiambia Saluti5 kuwa hadi sasa wameadhimia kukubali kazi ya Mungu na hawatarajii kuufanyia upasuaji mwili wa marehemu ili kujua chanzo cha kifo chake.
Maisha yake katika siku za hivi karibuni:
Ndugu wa marehemu wanasema katika siku za hivi karibu, Aisha alikuwa akiondoka nyumbani kwao Kigamboni asubuhi na kusema anaelekea kwenye mazoezi ya Twanga Pepeta kwaajili ya onyesho la miaka 16 ya Luizer Mbutu.
Lakini kiongozi wa madansa wa Twanga, Danger Boy ameiambia Saluti5 kuwa Aisha Madinda hajawahi kuonekana kwenye mazoezi ya bendi yao.
Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luzier Mbutu naye amekiri kuwa licha ya Aisha Madinda kumwahidi mara kadhaa kwa njia ya simu kuwa atashiriki mazoezi, lakini hakuwahi kutokea hata mara moja.
Mazishi yake:

Mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mwananyamala na mazishi yatafanyika Kigamboni kesho saa 10.
 Amida Mbegu dada wa Aisha Madinda
 Feisal mtoto wa kwanza wa Aisha Madinda
 Marafiki wa marehemu Aisha Madinda
Dada mweye fulana yenye mistari nyeupe na nyekundu ndiye Samira aliyemwokota Aisha Madinda
 Luizer Mbutu na Steve Nyerere
Baadhi ya viongozi wa Aset inayomiliki Twanga Pepeta, Omar Baraka (kushoto) na Hassan Rehani
 Baadhi ya wasanii wa Twanga Pepeta waliofika Mwananyamala Hospital

AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA KIFO CHA UTATA, MWILI WAKUTWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Aliyekuwa mnenguaji Mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Aisha Madinda, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha na mwili wske umegundulika ukiwa umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala mchana huu.

Akizungumza na kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.

“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Alisema Asha Baraka

Naye Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu, alisema kuwa, ''Aisha Madinda amefariki dunia, kifo cha utata na mwili wake umekutwa hospitali ya mwananyamala, haijulikani aliyeupeleka,

Bado Uongozi wa Twanga tupo eneo la tukio hapa hospitani tukisubiri majibu kuhusu utata huo, je ni nani aliyepeleka mwili huo hospitalini hapa kwani inaonyesha alifilishwa hapa akiwa tayari amekwishafariki''.alisema Hassan
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina

AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA

breaking-news-alert-graphic-new-as-of-3-21-11-27279469-e1351416678191
Taarifa ambayo imetolewa kupitia Clouds FM December 17, 2014 mchana ni kuhusu kifo cha aliyekuwa mnenguaji maarufu kwenye familia ya muziki wa dansi Tanzania Aisha Mohamed Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’.
aishamadindaChanzo cha kifo chake bado hakijafahamika lakini taarifa za awali zinasema alipelekwa hospitali ya Mwananyamala akiwa tayari amefariki, taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu itakufikia punde kupitia millardayo.com muda mfupi baada ya kunifikia.

Tuesday, December 16, 2014

Tahadhari:'Hatari za urembo bandia'

Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii
Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.
Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.
'Uasi mkubwa'
Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa
Katika nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi ya 'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.
''Msisitizo unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema ''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
'Gharama si mchezo'
Baada ya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti, mawnamke huyu alipata na titi moja kubwa na lengine ndogo
Kim Bok-soon alitumia Won milioni 30 (£17,320) kwa jumla ya upasuaji mara 15 kwenye uso wake katika kipindi cha siku moja na baadaye akagundua kuwa daktari wake hakuwa mpasuaji wa kuongeza urembo bandia mwilini ambaye alimhadaa Kim BoK-Soon kutumia won (17,320) kufanya upasuaji mara 15 kwenye uso wake.
Sehemu ya shida ni kuwa upasuaji wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa hivyo unawaalika madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale waliohitimu katika nyanya zingine za utabibu.
Inadaiwa kuwa taratibu zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi moja kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati mgonjwa wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na kuwacha kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.
Juu ya hiyo, iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza urembo bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.
Kwa uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.
'Biashara kubwa'
Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandia
Lakini wao wanapigana na mseto huu, Upasuaji una faida sana, hata una bei ambazo zinadhoofisha upasuaji huo Marekani na Ulaya. Ni biashara kubwa sana huko Gangnam, hapa katika Seoul, bei ya "kurekebisha jicho" ni dola 1500 na ni shughuli inayochukua dakka 30 tu. hiyo huongezeka hadi dola 11,000 kwa upasuaji wa kurekebisha sura.
Lakini labda watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa Korea Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia kisu cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye mahakama.
Malkia aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa upasuaji wa kukuza kifua ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani upasuaji huo ulifanya titi lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.
Analaumu madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ". Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama madawa ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."
Na madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji" Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni juu yako mwenyewe.

Ujio Mpya wa Johari, Mjasiriamali Anaeuza Ndizi



Ujio Mpya wa Johari, Mjasiriamali Anaeuza Ndizi
Muigizaji mkongwe wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amabae pia ni mkurugezi wa kampuni ya RJ ambayo inajihusisha na utengenezaji wa filamu hapa nchini. Hivi karibuni kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM aliweka picha hii,akionekana kichwani amejitwisha beseni lenye ndizi, yani kama mdada muuza ndizi anaetembea majumbani.Kwenye picha hii Johari aliandika kuwa hii ndio kazi yake mpya inayokuja japokuwa hakusema ni lini itakoka na hata jina la filamu hiyo hakulisema.
Johari aliandika maneno haya;
"Ujio mpya wa johari nikiwa mjasiriamali nauza ndizi dayana, we saka… mi nasaka pesa. heshima ya mtu pesa baby baby makelele".
Johari ni moja kati ya waigizaji wakike wenye uwezo na uzoefu mkubwa zaidi kwenye tasnia hii ya filamu na hivyo kujijengea heshma miongoni mwawaigizaji wakongwe na hata wapya huku mashabiki wake  wengi wakiendelea kumuunga mkono kwa kazi zake nzuri zenye ubora.
Mashabiki wengi walionyesha kuisubiri kwa hamu kaizi hii mpya, kwani ni kitambo sasa tangu Johari atoe mzigo mpya.

Sunday, December 14, 2014

MALIA OBAMA ABEBESHWA UJAUZITO

Baada ya story kuhit sana kwenye vyombo vya habari kwamba mtoto wa rais Barack Obama, Malia Obama kuwa ni mjazito zimethibitishwa na yule alikuwa akishutumiwa kuwa ndie aliyempatia ujazito huo  

Mitandao mikubwa ya nchini marekani imekuwa ikiripoti kuwa mtoto wa raisi huyo amekuwa akiwa na tabia za kutoka usiku kwenda kwa huyu mwanaume anayesadikiwa na ni mpenzi wake na na hujui funika koti la ngozi likiwa ni mali ya mwanaume huyo ambaohutoka ikulu usiku huo na kwenda kupunga hewa.

Mama yake na Malia Obama, 
Michelle Obama alipofanya interview na moja ya vituo vikuwa vya Tv nchini marekani alikuwa na haya ya kusema   

“Teen pregnancy is common in our family on her father’s side of course.My mother-in-law had Barack when she was 18, so I see where Malia gets it from. I’m just so excited to decorate the nursery. The White House hasn’t seen a baby since oh, 1884 or so.”

Alimaliza kwa kusema hivyo sasa na na wengine pia ndio imekuwa sehemu ya kujipatia umaarufu mtizame huyu

 











Cheni (Mkufu) wa LULU wazua utata. Wengi wasema ni kama wa IDRIS. Wachache wadai eti ni FREEMASONS



Cheni (Mkufu) wa LULU wazua utata. Wengi wasema ni kama wa IDRIS. Wachache wadai eti ni FREEMASONS
Baada ya mwanadada LULU kutupia picha yake mpya kwenye mtandao akiwa amevaa cheni ama mkufu  mpya shingoni mwake, maswali kadhaa ya wadau yameanzaje kujitokeza kuhusu cheni hiyo pamoja na maana yake.
Huku kukiwa bado kuna vuguvugu la ushindi wa Tshs.  MILLIONI 500 za kijana Idris toka jumba la BIG BROTHER na lulu akiwa ni mmoja wa watu wakubwa sana waliokuwa wanawahimiza wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na mipaka yake kumpigia kura kijana huyu ili ashinde, maswali Kadhaa yamejitokeza kuhusiana na mkufu huo ulioko kwenye shingo laini ya mrembo LULU.
1. Swali kuu la kwanza?
Je, LULU kanununua mkufu wenye alama hiyo ili ufanane na ule wa Idris aliyeshinda million 500? kama mpango yakinifu wa kujiweka karibu na ‘Millionea’ huyo?
2. Swali kuu la pili?
Lulu kajiunga FREEMASONS? Mbona mkufu wake huo una alama zao zile zaoo?
Tusaidie ndugu msomaji kwa maoni yako hapo chini…

Wednesday, December 10, 2014

TEAM WEMA Wapumua,Project Mpya Ya Wema



TEAM WEMA Wapumua,Project Mpya Ya Wema
  • TEAM WEMA Wapumua,Project Mpya Ya Wema 1
Makundi ya mashabiki mitandaoni maarufu kama TEAMS yamekuwa ni sehemu ya maisha ya mtandaoni ya wasanii na watu maarufu wengi hapa nchini. Linapokuja swala ya ushabiki na mada nzito team hizi  huvutana kwa kutupiana maneno na wakati mwingine hadi maneno makali.
Siku za hivi karibuni baada ya mwigizaji Wema Sepetu alipoachana na mpenzi wake Diamond Platnum, na badaye Diamond kuamua kutoka na mwanamama Zari kutoka nchini Uganda, Mashabiki (TEAM) wa Diamond na wale wanaomponda Wema Sepetu wamekuwa kwakiasi kikubwa wakiwatupia maneno na vijembe wale mashabiki wa Wema (TEAM WEMA), kwa picha na maneno.kiasi ambacho TEAM WEMA kuonekana kama” LOSSERS”.
Lakini leo hii upepo umebadilika huko mitandaoni na  TEAM WEMA wanaonekana kuwa na nguvu zaidi, baada ya mwigizaji Wema Sepetu kuachia baadhi ya picha akiwa nchini Ghana akifanya  kazi na Van vicker ambae ni msanii mkubwa hapa Afrika.
Team Wema wamepongeza sana juhudi za mwigizaji huyo kutaka kuivusha tasnia ya filamu hapa nchini na kuipeleka kimataifa hivyo wanataka Le Projectii iemdelee
Bongomovies pia inampongeza na kunampa moyo  katika juhudi zake hizi za kukuza tasnia yetu.Hiyo ni moja ya picha za project hiyo mpya

Tuesday, December 9, 2014

MAANDALIZI YA KUADHIMISHO MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA

MAANDALIZI YA KUADHIMISHO MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA

Askari wa jeshi la polisi wav kuzuia ghasia FFU wakiwa katika gwaride la maandalizi ya siku maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Wato wa halaiki  wakionyesha umahili wao wakati wa maandalizi  ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru iliyofanyika leo

Wato wa halaiki  wakionyesha umahili wao wakati wa maandalizi  ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru iliyofanyika leo 


Wato wa halaiki  wakionyesha umahili wao wakati wa maandalizi  ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru iliyofanyika leo 

Wato wa halaiki  wakionyesha umahili wao wakati wa maandalizi  ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru iliyofanyika leo 

Askari wa jeshi la polisi wav kuzuia ghasia FFU wakiwa katika gwaride la maandalizi ya siku maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Askari wa jeshi la polisi wav kuzuia ghasia FFU wakiwa katika gwaride la maandalizi ya siku maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam


Askari wa jeshi la polisi wav kuzuia ghasia FFU wakiwa katika gwaride la maandalizi ya siku maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

BENDERA YA UHURU KATIKA MLIMA KILIMANJARO

PICHA: MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA

Tarehe December 9, 2014
Maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika yanafanyika hivisasa katika uwanja wa uhuru jijini Dares salaam.
Maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika yanafanyika hivisasa katika uwanja wa uhuru jijini Dares salaam.
Vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho hayo.
Vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho hayo.
Mamia ya wananchi wajitokeza katika maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika.
Mamia ya wananchi wajitokeza katika maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika.
Wananchi waliohudhuria maadhimisho ya uhuru ya uhuru.
Wananchi waliohudhuria maadhimisho ya uhuru ya uhuru.
Jukwaa kuu ambapo viongozi mbalimbali wanaingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya uhur wa Tanganyka.
Jukwaa kuu ambapo viongozi mbalimbali wanaingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya uhur wa Tanganyka.
Maelfu ya wanachi wajitokeza katika maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika leo jijini Dares salaam.
Maelfu ya wanachi wajitokeza katika maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika leo jijini Dares salaam.
Vikosi vya ulinzi katika maadhimisho hayo.
Vikosi vya ulinzi katika maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika yanafanyika hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ingia katika historia ya nchi yetu jitokeze kuipigia kura Katiba inayopendekezwa”.
Mtandao  wa  Hivisasa utaendelea kukujulisha kila kinachojiiri katika maadhimisho hayo.

Yaliyojiri sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru: Jumanne, Tarehe 9 Desemba, 2014




Leo ni mwaka wa 53 tangu upatikane uhuru wa Tanzania bara(Tanganyika) kutoka kwa muingereza, kama ilivyo ada ya miaka mingi, 9 Desemba huwa kuna sherehe za kuadhimisha siku hii na leo ntajitahidi kuwaeleza kinachojiri uwanja wa Uhuru, Tuwe pamoja.
===================



Sherehe zimeshaanza na sasa hivi mshehereshaji anatambulisha viongozi mbali mbali wa gwaride. Viongozi mbali mbali wa kitaifa na wageni waalikwa washafika ndani ya uwanja wa Uhuru. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Kikwete ndio anasubiriwa ili maadhimisho ya sherehe ya Muungano wa Tanzania uanze.

- Rais wa awamu ya pili mh. Ali Hassan Mwinyi ndio anaingia kwenye uwanja wa uhuru akiwa kaongozana na mke wake.

- Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idi anawasili kwenye eneo la tukio akiwa kaongozana na wake zake wawili.

- Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na rais wa Bunge la SADC anawasili kwenye uwanja wa tukio.

- Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mh. Seif Sharif Hamad anawasili

- Waziri mkuu wa JMT mh. Peter Kayanza Pinda anawasili kwenye uwanja wa Uhuru.

Anaesubiriwa sasa na raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mh Ali Shein, anaingia na kuelekea kwenye sehemu yake iliyotengwa baada ya kusalimiana na meza kuu.

Msemaji anaendelea kutambulisha uongozi wa gwaride leo

Anaewasili ni mke wa raisi, mama Salma Kikwete

Msemaji anatoa ratiba ya leo na raisi ataondoka viwanjani mishale ya saa sita baada ya maadhimisho

Raisi wa Jamhuri anaingia ndani ya uwanja wa uhuru na watu wanamshangilia sana hapa, anaenda kwenye jukwaa lilitengwa kusubiri wimbo wa taifa.

Rais anaelekea kukagua gwaride la vikosi vilivyopo hapa uwanjani, raisi anasalimiana na jukwaa kuu na kukaa kwenye kiti chake

Sasa gwaride linapita mbele ya rais. Gwaride linatoka baada ya kumaliza na inafata watoto wa alaiki wapatao 1040, pia kuna watoto wa sekondari wapatao 1,000. Wanatengeneza maumbo mbalimbali kama V na daraja kuashiria mafanikio awamu ya nne kwenye ujenzi wa madaraja pia wametengeneza alama ya kuashiria mawimbi.

Wanatengeneza umbo la maabara kuashiria juhudi za serikali kuinua masomo ya sayansi na mfano wa nwalimu alie darasani kuwaelekeza wanafunzi kuchanganya kemikali, sasa wanatengeneza umbo la ramani ya Tanzania kueleza juhudi za serikali kudhibiti magonjwa ikiwemo Ebola. Baada ya ramani wanatengeneza umbo la mlima Kilimanjaro na kuweka bendara ya Tanzania juu kuimba wimbo.

Sasa wanaimba na kucheza ngoma, halaiki wamemaliza na sasa wanatoka nje.

Sasa kinachofata ni kikundi cha kwaya kutoka Mwanza, Ngoma kutoka Kaskazini Pemba ndio waliopo sasa.

Sasa ni ngoma ya Mbangamojo kutoka Bujonde Kyela na imemaliza burudani, na sasa unakuja wimbo maalumu ulioimbwa na kikundi cha usalama.

Kikundi maalumu cha usalama kimemaliza, kwa mujibu wa ratiba sherehe zimeisha na Rais Kikwete anaondoka uwanjani.

Monday, December 8, 2014



SHEREHE ZA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA DMV

Sherehe ya kusherehekea miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 6, 2014 ndani ya Hotel ya Sheraton iliyopo katikati ya jiji la Silver Spring, Maryland, na kuhudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali na wengine wakitokea Tanzania.
Katika sherehe hiyo iliyoratibiwa na maporomota wakubwa nchini Marekani Phanuel Ligate, Innocent Batamilwa na Dickson Mkama wakishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani huku mgeni rasmi akiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na baadae sherehe hizi zilinogeshwa na msanii wa Bongo Flava Diamond Platnumz anayekimbiza sasa hivi kwenye tasnia hiyo ya Bongo flava  Tanzania na nje ya Bongo.
Diamond aliyeambatana na wacheza show wake akiwemo Dj Romy Jones yeye mwenyewe aliwasili Washington, DC siku hiyo ya Jumamosi Desemba 6, 2014 na baadae kukata kiu ya mashabiki wake na kuwapa burudani ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambao kwa mara ya kwanza katika historia nchini Marekani umesherehekewa na mwanamuziki kutoka Bongo mwenye jina kubwa .
Katika sherehe hizo pia alikuwepo Mbunge wa viti maalumu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Leticia Nyerere na Balozi mstaafu Mhe. Mustafa Nyang'anyi. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiingia ukumbini kulia ni Afisa Suleiman Saleh wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Mbunge viti maalum CHADEMA mhe. Leticia Nyerere.Balozi Liberata Mulamula akibadilishana mawili matatu na Balozi Mstaafu Mhe. Mustafa Nyang'anyi. Wimbo wa TaifaKutoka kushoto ni Mhe. Liberata Mulamula, mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Innocent Batamulwa. na Mbunge viti maalum CHADEMA mhe. Leticia Nyerere.

Sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara yafana DMV

Sherehe ya kusherehekea miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 6, 2014 ndani ya Hotel ya Sheraton iliyopo katikati ya jiji la Silver Spring, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali na wengine wakitokea Tanzania.   Katika sherehe hiyo iliyoratibiwa na maporomota wakubwa nchini Marekani Phanuel Ligate, Innocent Batamilwa na Dickson Mkama wakishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani huku mgeni rasmi akiwa...


SHEREHE YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA DMV‏

 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiingia ukumbini kulia ni Afisa Suleiman Saleh wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.  Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Mbunge viti maalum CHADEMA, Mhe. Leticia Nyerere.…

(Yesterday)

Vijimambo

PICHA ZINGINE SHEREHE YA UHURU WA TANZANIA BARA DMV

Dj Seif akifanya vitu vyake kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 6, 2014 Sheraton ya Silver Spring, Maryland mchini Marekani.Watanzania wakijumuika pamoja kwenye sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Watanzania wakiwa kwenye sherehe ya Uhuru wa miaka 53 Sheraton hotel ya Silver Spring, Maryland.Nyamy katika picha.Taji na mama mwenye nyumba wake.Aziz na mdhamini wa pendo lake.Rich akiwa na barafu ya moyo wake.Picha zote na Ayoce Mbullu mwakilishi...