Aliyekuwa
mnenguaji Mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Aisha
Madinda, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha na mwili wske
umegundulika ukiwa umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala mchana huu.
Akizungumza na kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta,
Asha Baraka, alisema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona
kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda
kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo
walipogundua ni yeye.
“
Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya
kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha
sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa
simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala, hata
sielewi nini kimetokea”. Alisema Asha Baraka
Naye Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu, alisema kuwa, ''Aisha Madinda amefariki dunia, kifo cha utata na mwili wake umekutwa hospitali ya mwananyamala, haijulikani aliyeupeleka,
Bado Uongozi wa Twanga tupo eneo la tukio hapa hospitani tukisubiri majibu kuhusu utata huo, je ni nani aliyepeleka mwili huo hospitalini hapa kwani inaonyesha alifilishwa hapa akiwa tayari amekwishafariki''.alisema Hassan
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina
No comments :
Post a Comment